Jumanne 22 Julai 2025 - 04:08
Njia ya uokovu wa Umma katika zama za fitna imo katika mafundisho ya subira na munajat ya Imam Zaynu l-‘Ābidīn (as)

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Sayyid Sajid Ali Naqavi, katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya siku ya shahada ya Imam Zaynu l-‘Ābidīn (as) amesisitiza kuwa: Mtukufu huyo kutokana na subira na munajat aliweka ramani ya mwamko na kusimama imara, na kurejea katika mafundisho yake ni jambo la dharura katika maisha kwa ajili ya umma wa Kiislamu kwenye zama hizi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Sayyid Sajid Ali Naqavi, Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia nchini Pakistan, katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya siku ya shahada ya Imam Zaynu l-‘Ābidīn (as), huku akielezea nafasi ya kihistoria na kiroho ya mtukufu huyo katika kubainisha na kuthibitisha mafundisho ya harakati ya Ashura, ameeleza wazi kuwa: Imam Sajjad (as) kutokana na subira, dua na uelimishaji, katika giza totoro la historia, aliweka wazi njia ya kuamsha umma na kusimama dhidi ya batili; hivyo basi, kurejea katika mafundisho ya Imam huyo mkubwa katika mazingira nyeti ya zama hizi ni jambo lisilopingika kwa ajili ya uokovu na heshima kwa umma wa Kiislamu.

Akiendelea kuashiria hali ngumu sana na nzito ambayo Imam Zayn al-‘Ābidīn (as) aliipitia katika maisha yake, amekumbushia kuwa: Mtukufu huyo hakuwa tu shahidi wa matukio ya kuhuzunisha na ya kuumiza moyo ya Karbala, bali pia baada ya matukio hayo, katika kipindi cha kifungo na utumwa, akiwa katika hali ya kudhulumiwa lakini mwenye msimamo thabiti, aliufikishia ulimwengu ujumbe wa mapambano ya Ashura, Imam Sajjad (as) aliishi katika hali ambayo kulikuwa na ukandamizaji wa hali ya juu, dhulma, upotovu wa kidini na tamaa ya madaraka, lakini kutokana na subira, hekima na basira, aliweza kuweka na kuendeleza misingi ya fikra na maadili ya harakati ya Husseinia.

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistan ameongeza kuwa: Imam wa nne wa Mashia aliingia uwanjani kwa kutumia silaha tofauti; silaha ambayo haikuwa ya upanga wala nguvu za misuli, bali ni silaha ya dua, munajat, hekima, malezi na uelimishaji. Kwa njia ya maneno yake yenye mwanga na undani mkubwa, alifikisha ndani ya nafsi maana ya juu ya tauhidi, uchamungu wa kweli, uadilifu na heshima ya mwanadamu, na akaamsha dhamira zilizolala, japokuwa Yazid na mfumo wa dhulma wa zama hizo walitaka kuizima sauti ya haki, Imam Sajjad (as) kwa mbinu ya kimungu na ya busara, si tu kwamba hakuzima sauti ya Karbala, bali aliigeuza kuwa mkondo wa kudumu wa uelimishaji na uamsho katika historia.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha